Premier Projects kuzindua Kampeni ya Michezo kwa Wote

Imechapishwa: 1 Februari, 2021

Kampeni ya Sekta ya jamii ya Premier Loto itasaidia klabu za michezo ndogo ndogo na kuboresha miundo mbinu ya jamii

Premier 6

Premier Projects imetangaza uzinduzi wa Kampeni yao mpya ya – Michezo kwa Wote.

Michezo kwa Wote itahakikisha Premier Projects inaboresha na kujenga miundo mbinu mipya ya michezo, kama vile viwanja vya mpira wa kikapu na viwanja vya mpira wa miguu. Hivi vitatosheleza na kuifikia na jamii nzima.

Na pia, Premier Projects itatoa msaada kwa klabu ndogo ndogo za mpira wa miguu ndani ya Afrika. Udhamini utasaidia kuboresha viwango vya timu na ushindani, kwa kutoa msaada wa kukabiliana na changamoto za kifedha.

Premier Projects na sekta ya Jamii ya Premier Loto, imefanya kazi kwenye nchi kama vile Malawi, Ghana, Cameroon, Angola na Mali kwa miezi 12 iliyopita. Miradi yao imehusisha kuboresha viwanja vya mpira wa wavu, mpira wa kikapu na tennisi.

Msemaji wa Premier Projects alisema: “Michezo kwa Wote inasimamia Imani yetu ya msingi; watu wote wanastahili kupata vifaa bora vya michezo ila wafurahi na kutunza afya zao.

Tunaona Fahari kubwa ya kazi tuliyoifanya kuboresha miundo mbinu ya michezo inayofikika. Michezo kwa Wote ndio kauli mbiu ya maendeleo yote haya.”

Shughuli zote zinazohusiana na michezo za Premier Projects zitaangukia kwenye matangazo ya Michezo kwa Wote. Hii inajumlisha uzinduzi ujao wa miundo mbinu nchini Cameroon na Ghana, ikiwemo na udhamini wa kusisimua wa klabu za mpira ndani ya Afrika.

Kwa taarifa Zaidi juu ya Michezo kwa Wote, tembelea kurasa zetu za Premier Projects kwenye mtandao wa Facebook, Instagram na YouTube.