SERA YA FARAGHA

Tumejitolea kulinda taarifa zako za kibinafsi, Tumeunda sera hii ya faragha ili kukufahamisha taarifa tunazokusanywa unapotumia huduma zetu, kwa nini tunakusanya taarifa hizi na jinsi tunavyotumia taarifa tulizokusanya.

Tafadhali zingatia kuwa sera hii ya faragha inaafikiwa baina yako na kampuni ya Premier Bet kama ilivyojelezwa kwenye Sheria na Masharti('Premier Bet', ‘Sisi’, ‘kwetu’ au ‘Yetu’, kama inavyofaa). Huenda tukafanya marekebisho kwa sera hii ya faragha mara kwa mara na tutakufahamisha kuhusu mabadiliko hayo kwa kuchapisha masharti yaliyorekebishwa kwenye Majukwaa Yetu. Tunapendekeza uwe ukirejelea Sera ya Faragha mara kwa mara.

TAARIFA ZINAZOKUSANYWA

Tunachukulia taarifa ambazo zinaweza kutumiwa kumtambua mtu, ikiwemo, bila ya kujikita tu kwa, jina la kwanza na la familia, tarehe ya kuzaliwa, taarifa kuhusu kadi ya mkopo, anwani ya nyumbani na mahali pa kuishi, anwani ya barua pepe, nambari ya simu au taarifa nyingine za mawasiliano kuwa taarifa za kibinafsi (‘Taarifa za Kibinafsi’). Unaweza kuombwa kutoa taarifa za kibinafsi unapotumia tovuti yetu, unapojisajili kwa akaunti au unapotumia Huduma zetu. Taarifa za Kibinafsi Tunazokusanya zinaweza kujumuisha taarifa kama vile: Taarifa za mawasiliano (ikiwemo nambari ya simu), taarifa za kutumiwa barua kutoka ughaibuni, taarifa zinazohusu malipo, historia ya shughuli, mapendeleo katika matumizi ya tovuti, pamoja na maoni kuhusu Huduma zetu. Taarifa hisi tunazihifadhi kwenye sava zilizoko Malta na kwingineko kadri muda unavyosonga. Zaidi ya hayo, unapotangamana na Huduma zetu, sava zetu huweka kumbukumbu ya shughuli mahususi kwako ambayo hukusanya taarifa fulani za kiusimamizi na matumizi ikiwemo: IP address yako, wakati wa kuingia kwenye tovuti, tarehe ya kuingia kwenye tovuti, gombowavu ulizotembelea, lugha unayotumia, matatizo ya programu yaliyoripotiwa na aina ya kisakuzi iliyotumiwa. Taarifa hizi ni muhimu kwa utoaji wa Huduma bora. Hatukusanyi taarifa kukuhusu kwenye matumizi ya Huduma zetu bila Wewe kujua.

NJIA ZA KUKUSANYA NA KUCHAKATA DATA

Huenda tukakusanya data fulani moja kwa moja kama ilivyojadiliwa hapo juu na tukapokea taarifa za kibinafsi kukuhusu ambapo unatoa taarifa hizi kupitia kwa Huduma au mawasiliano na maingiliano mengine nasi. Huenda pia tukapokea Taarifa za Kibinafsi kutoka kwa watoaji wa huduma hizi na wauzaji mtandaoni, pamoja na kutoka kwa orodha za wateja zinazopatikana kutoka kwa washiriki wa nje kwa mujibu wa sheria. Isitoshe, Tunaweza kutumia huduma za washiriki wa nje ili kutoa msaada wa kiufundi, Kuchakata shughuli zako mtandaoni na kutunza Akaunti Yako. Tutaweza kupata taarifa zozote unazotoa kwa washiriki kama hao, watoaji wa huduma pamoja na washiriki wa nje wanaotoa huduma za biashara mtandaoni na tutazitumia taarifa hizi za kibinafsi kama ilivyoelezwa kwenye Sera hii ya Faragha hapo chini. Taarifa hizi zitatolewa tu kwa washiriki kutoka nje ya Kampuni kuambatana na Sera hii ya Faragha. Tunachukua hatua kuhakikisha kuwa Makubaliano yetu na washiriki wanaotoa huduma kutoka nje pamoja na wauzaji mitandanoni yanalinda usiri Wako.

MATUMIZI YA TAARIFA

Tunatumia Taarifa za Kibinafsi tunazokusanya kutoka kwako ili kutoa Huduma, kutoa msaada kwako, kuendesha shughuli za uthibitishaji wa utambulisho na usalama, kuchakata shughuli zako mtandaoni, kukusaidia kushiriki mashindano ya washiriki kutoka nje, kutimiza mahitaji maalum ya kibiashara na kwa matumizi mengine yanayohusiana na uendeshaji wa huduma zetu. Kutokana na hayo, tunaweza kutoa Taarifa zako za Kibinafsi kwa washiriki wetu walioteuliwa kwa uangalifu (hii itajumuisha washiriki wengine ambao huenda washiriki husika wameingia mkataba nao kuhusu ushiriki wa data).

Tunaweza pia kutumia Taarifa zako za Kibinafsi ili kukupa: (a) ofa za mashindano na taarifa kuhusu bidhaa na huduma Zetu; na (b) ofa za mashindano na taarifa kuhusu bidhaa na huduma za washiriki wetu walioteuliwa kwa makini, ili kutuwezesha kukupa bidhaa na huduma anuwai pamoja na kuimarisha utoaji wa huduma kwako kama mteja wetu. Unatupa kibali cha kuwafahamisha watumiaji wengine wa Tovutu yetu walio na akaunti na walio na anwani yako ya barua pepe katika hifadhi zao za mawasiliano katika barua pepe zao, kwamba barua pepe husika tayari imesajiliwa kwa Akaunti. Mara kwa mara huenda tukaomba taarifa kutoka Kwako kupitia kwa utafiti au mashindano. Kushiriki katika mahojiano au mashindano haya ni kwa hiari yako, na hivyo basi una uhuru wa kutoa ama kutotoa taarifa kama hizo. Taarifa zitakazoombwa zinaweza kuhusisha taarifa za mawasiliano (kama vile jina, anwani ya mawasiliano na nambari ya simu), pamoja na taarifa za kidemografia (kama vile anwani ya posta au umri wako). Kwa kukubali kushiriki zawadi au ushindi kutoka Kwetu, unakubali jina na sura yako kutumiwa kwa matangazo ya kibiashara na katika utangazaji wa mashindano bila ya kukulipa chochote, isipokuwa pale sheria inakataza. Isipokuwa pale ambapo umechagua kutopokea taarifa za mashindano, Tunaweza pia kutumia taarifa za kibinafsi (ikiwemo barua pepe yako na nambari ya simu) kukupa taarifa zaidi kuhusu bidhaa zetu, huduma zetu, mashindano, michezo mingine ya kamari, huduma na bidhaa kutoka kwa washiriki wetu kutoka nje tuliowateua kwa makini.

KUPIGA SIMU

Simu unazopiga au kupigiwa kutoka kwa Kituo chetu cha Kuwahudumia Wateja zinarekodia kwa ajili ya utoaji mafunzo na kwa sababu za kiusalama pamoja na utatuzi kwa masuala yoyote yanayoibuka kutokana na huduma unayopokea.

UFICHUZI AMBAO HAUJALINDWA

Huenda tukatoa taarifa zako za kibinafsi iwapo tunahitajika kufanya hivyo na sheria, au iwapo tunaamini kwamba hatua hiyo ni muhimu ili: (1) Kutimiza mahitaji yoyote ya kisheria Kwetu, tovuti Zetu wowote au huduma au katika hali ambapo tuna wajibu kama huo kisheria; (2) kukinga na kulinda haki zetu au mali yetu; au (3) kufanya hivyo ili kulinda usalama wa watumiaji wengine wa huduma zetu au usalama wa umma. Iwapo, kwa uamuzi wetu, Unapatikana ulidanganya au ulijaribu kututapeli, kutapeli Kampuni, au mtumiaji mwingine wa huduma zetu kwa njia yoyote ikiwemo, bila ya kujikita kwa, utapeli wa mchezo au utapeli wa malipo, au iwapo tunashuku ulipata malipo yasiyofaa, ikiwemo matumizi ya kadi za mkopo zilizoibiwa, au shughuli nyingine ya kitapeli (ikiwemo kukatiza malipo yaliyokwishafanywa) au shughuli iliyokatazwa (ikiwemo utakatishaji wa pesa) tuna haki ya kutoa taarifa hizi (pamoja na jina lako na utambulisho) kwa watoaji wengine wa huduma za kamari mtandaoni, benki, kampuni za kadi za mkopo na asasi nyinginezo. (4) Kwa ajili ya utafiti ili kuzuia uraibu, data inaweza kutolewa bila kukutambulisha kwa asasi zinazohusika.

UPATAJI

Unaweza ‘kujiondoa’ kupokea mawasiliano ya matangazo ya mashindano kwa ama kuchagua kujiondoa wakati nafasi hiyo imetolewa mtandaoni au huduma zetu au kwa barua pepe utakayopokea kutoka kwetu, au wakati wowote kwa kututumia barua pepe, au kwa kutuandikia kwa Tanzania: Premier Bet, Sukuma Street, Dar es Salaam. Zaidi ya hayo, unaweza kuwasiliana Nasi kwa anwani hii iwapo: 1) Unataka kuhakikisha usahihi wa Taarifa zako za Kibinafsi tulizokusanya kwako; 2) Ungependa kuimarisha taarifa zako za kibinafsi; na/au 3) Una malalamishi yoyote kuhusiana na matumizi yetu ya taarifa zako za kibinafsi. Iwapo utaomba, tuta (a) sasisha taarifa yoyote uliyotupatia, almuradi utatoa ithibati tutakayohitaji ili kufanya marekebisho hayo, au (b) kutambua taarifa yoyote ili kuzuia matumizi ya baadaye katika matangazo yetu. Hata hivyo, ni muhimu utambue kuwa, hakuna chochote katika Sera hii ya Faragha kinachotutinga kuzuia Taarifa zako za Kibinafsi tunapohitajika kufanya hivyo kisheria.

KIBALI CHA KUTUMIA WATOAJI HUDUMA ZA KIELEKTRONIKI

Ili kushiriki michezo ya pesa katika Huduma zetu, Utahitajika kutuma pesa kwetu na kupokea pesa kutoka Kwetu. Huenda tukatumia washiriki wa nje wanaowezesha malipo kielekroniki na/au asasi za kifedha (‘ESPs’) ili kuchakata miamala kama hiyo ya kifedha. Kwa kukubali Sera hii ya Faragha, Unatoa kibali cha kutoa taarifa za kibinafsi ambazo zinahitajika kuwezesha uchakataji wa shughuli hizi kwa ESPs, ikiwemo, inapohitajika, kutoa taarifa nje ya nchi yako. Tunachukua hatua kuhakikisha kwamba Makubaliano yetu na ESPs yanalinda faragha Yako.

KIBALI CHA UKAGUZI WA KIUSALAMA

Tuna haki ya kuendesha uchunguzi wa kiusalama wakati wowote ili kuthibitisha utambulisho wako, umri, data ya usajili uliyotoa pamoja na kuthibitisha matumizi yako ya Huduma zetu na miamala yako ya kifedha kuhakikisha hujakiuka Sheria na Masharti yetu na hujakiuka sheria zinazohusika. Kwa kukubali Sheria na Masharti yetu, unatoa kibali kwetu, kwa wafanyakazi wetu, maajenti na wasambazaji kutumia Taarifa zako za Kibinafsi na kutoa taarifa hizi kwa washiriki wa nje kwa ajili ya kuthibitisha taarifa ulizotupatia katika harakati za kutumia Huduma zetu, ikiwemo, inapohitajika, kutoa taarifa nje ya nchi Yako. Uchunguzi wa kiusalama unaweza kujumuisha, bila ya kujikita kwa, kuitisha ripoti ya kifedha na/au vinginevyo kuthibitisha taarifa ulizotoa kwetu kwa kuzilinganisha na hifadhidata za washiriki kutoka nje. Zaidi ya hayo, ili kuwezesha uchunguzi huu wa kiusalama, unakubali kutupatia taarifa au hati kama tutakavyozihitaji.

USALAMA

Tunaelewa haja ya usalama wa taarifa na mbinu zinazohitajika ili kulinda taarifa. Tunahifadhi Taarifa zote za Kibinafsi tunazopokea moja kwa moja kutoka kwako kwenye kanzidata iliyowekewa nywila iliyopo kwenye mtandao wetu uliolindwa kwa programu za kisasa za kukinga virusilishi. Huduma zetu zinawezesha TLS (Transport layer Security) Toleo la 1.2. Tunachukua hatua kuhakikisha kwamba matawi Yetu, maajenti, washiriki na wasambazaji pia wanazingatia viwango vinavyohitajika vya usalama.

KULINDA WATOTO

Huduma hizi hazitarajiwi kutumiwa na watu walio na umri wa chini ya miaka 18 (au umri unaobainishwa kuwa utu uzima kisheria katika nchi mbalimbali). Mtu yeyote anayetoa taarifa zake kwetu kupitia kwa Huduma zetu zozote anatuhakikishia kwamba ana umri wa miaka 18 (au umri unaobainishwa kuwa utu uzima kisheria katika nchi mbalimbali) au zaidi. Ni sera yetu kujaribu kubainisha watoto ambao wanajaribu kutumia huduma Zetu ambayo inaweza kuhusisha kupata Taarifa za Kibinafsi ili kuzithibitisha. Iwapo tutabainisha kwamba mtoto amejaribu kutoa au ametoa taarifa za kibinafsi kupitia Huduma zetu, hatutakubali taarifa hizo na tutachukua hatua kuondoa taarifa husika kwenye rekodi Zetu.

UHAMISHAJI WA KIMATAIFA

Taarifa za Kibinafsi zinazokusanywa kupitia kwa Huduma zetu zinaweza kuhifadhiwa na kuchakatwa katika nchi yoyote ambapo tuna matawi au washirika, wasambazaji, ESPs au maajenti. Kwa kutumia Huduma zetu, Unakubali uhamisho wowote wa taarifa zako nje ya nje Yako (Ikiwemo kwa nchi ambazo hazijakaguliwa kuhakikisha zina sheria madhubuti kuhusu faragha). Hata hivyo, tunachukua hatua kuhakikisha kwamba maajenti wetu, matawi na wasambazaji wanazingatia viwango vyetu vya faragha bila ya kujali walipo.

UTENDAJI WA WASHIRIKI WA NJE

Hatuwezi kuhakikisha usalama wa taarifa zozote au picha ambazo unatoa kwa tovuti za washiriki wa nje ambazo zinaunganisha kwa Huduma zetu au taarifa zilizokusanywa na washiriki kutoka nje wanaosimamia programu tunazohusishwa nazo (iwapo inahusika) au programu nyingine yoyote, kwa kuwa tovuti hizi za washiriki wa nje zinamilikiwa na kuendeshwa kwa namna inayojisimamia kutoka kwetu. Taarifa zozote zizazokusanywa na washiriki hawa wa nje hazidhibitiwi na Sera hii ya Faragha bali zinadhibitiwa na sera ya faragha ya washiriki husika. Iwapo una maswali kuhusu matumizi na uhifadhi wa taarifa kwa washiriki wa nje, tafadhali soma sera ya faragha ya washiriki husika. Hatutakubali kuwajibikia kisheria utendaji, mienendo au sera za washiriki wa nje kama hawa, na hatutawajibikia yaliyomo au sera za faragha za tovuti kama hizi.

HATI YA KISHERIA YA KUKATAA

Huduma zetu hafanya kazi ’kama zilivyo’ (‘AS-IS’) na ‘kadri zinavyopatikana’ ‘KAMA INAVYOPATIKANA’ bila ya kukubali kuwajibika vyovyote kisheria. Hatutawajibikia matukio yaliyo nje ya udhibiti wetu wa moja kwa moja. Kutokana na mabadiliko ya mara kwa mara ya kiteknolojia na kibiashara, hatuwezi kukuhakikishia wala hatudai kuwa tutatoa huduma bila hitilafu yoyote kuhusiana na usiri wa taarifa zako za kibinafsi, na hatutawajibika kisheria iwapo kutatokea madhara yoyote ya moja kwa moja au kiuhusisho kutokana na matumizi au utoaji wa taarifa za kibinafsi.

MIUNGANO YA KIBIASHARA NA MATUKIO MENGINE YANAYOHITAJI UHAMISHO

Iwapo tutawahi kutangazwa kuwa tumefilisika, au tukawa hatuwezi kulipa madeni, au tukanunuliwa na mshiriki wa nje, au tukaungana na mshiriki wa nje, kuuza sehemu au mali yetu yote; au tukahamisha sehemu kubwa ya mali yetu au mali yote kwa mshiriki wa nje, tuna uhuru wa kutoa taarifa za kibinafsi na Taarifa nyingine zote ulizotoa kwetu kupitia kwa huduma zetu kwa wabia wetu wa kibiashara tulioungana nao. Kwa kukubali Sheria na Masharti ya matumizi, unatoa kibali kwa uhamisho kama huo wa taarifa.

KIBALI CHA SERA YA FARAGHA

Kwa kubonyeza ‘Wasilisha’ au “Ninakubali’ wakati wa mchakato wa usajili au kwa kuendelea kutumia huduma zetu baada ya sera hii ya faragha kuchapishwa (ile inayohusika), unakubaliana na Sera hii ya Faragha. Hii ndiyo Sera Yetu ya Faragha kwa kina chake na inatamalaki juu ya nakala ya awali. Sera hii ya Faragha inapaswa kusomwa pamoja na Sheria na Masharti yetu pamoja na kanuni nyingine husika zilizochapishwa katika Majukwaa Yetu. Huenda tukafanya marekebisho kwa Sera hii ya Faragha kutoka muda hadi muda na tutakufahamisha kuhusu mabadiliko hayo kwa kuchapisha masharti yaliyorekebishwa kwenye Majukwaa Yetu. Tunapendekeza uwe ukirejelea Sera ya Faragha mara kwa mara.