Premier Projects kuzindua Kampeni Ya Elimu kwa Wote

Imechapishwa: 13 Julai, 2021

Premier Projects kuzindua Kampeni Ya Elimu kwa Wote

Premier Projects wametangaza uzinduzi wa kampeni yao mpya ya kijamii ndani ya bara la Afrika; Elimu kwa Wote.

Elimu kwa Wote itahakikisha Premier Projects inawasaidia watu na taasisi za ndani ya bara zima katika masomo yao, miradi yao na Zaidi.

Hii itajumlisha kuandaa udhamini wa masomo, kulipia ada za wanafunzi, kutoa msaada wa vifaa vya elimu na kuwasaidia watu wazima kujifunza ujuzi mpya.

Tangazo la Elimu kwa Wote limewekwa sanjari na dondoo za mradi wa kwanza. Nchini Cameroon, Premier Projects wameingia mkataba na Chuo Kikuu cha Ngaoundere. Makubaliano yatahakikisha Premier Projects wanalipia masomo ya wanafunzi 12.

Msemaji wa Premier Projects alisema: “Tunayofuraha kutangaza Elimu kwa Wote. Kampeni hii imefanyiwa kazi kwa miezi mingi na tunaona Fahari kuiona inaanza kufanya kazi.

Elimu ni moja kati ya funguo muhimu katika kazi za jamii zetu. Tuna amini kwamba kuna watu wengi sana barani Afrika ambao wanashindwa kupata elimu kwa sababu zilizo njee ya uwezo wao. Kampeni hii inalenga kuwasaidia watu hao kutimiza ndoto zao.”

Katika Chuo kikuu cha Ngaoundere, Premier Projects watatoa msaada wa elimu kwa wanafunzi watatu katika vikundi vinne:

  • Wanafunzi bora wenye ulemavu wa kupooza viungo vya mwili
  • Wanafunzi bora waliopata Diploma/Stashahada bila kurudia mitihani
  • Wanafunzi bora wa masomo ya Sayansi na Teknolojia
  • Wanafunzi bora wa Kaskazini

Premier Projects italipa ada ya Chuo kikuu, ada ya malazi na vifaa vyote vya kitaaluma kama sehemu ya makubaliano. Wanafunzi watachaguliwa mwezi Oktoba, Novemba na Disemba 2021.

Elimu imekua sehemu ya Vipaumbele vya Premier Projects. Ndani ya Kinshasa, Sekta ya Jamii ya Premier Bet na Premier Loto, ilifanya Semina ya kuwasaidia wanawake kukuza biashara zao ndogo ndogo.

Ndani ya Guinea, Kampuni iliwalipia ada ya masomo wasichana 30 ambao walishindwa kulipia masomo yao hapo awali.

Mwaka 2020, Premier Projects walishirikiana na NGO, UKANI, kuwasaidia wanawake kujifunza ujuzi wa ushonaji nchini Malawi.

Elimu kwa Wote imekuja baada ya mafanikio ya Michezo kwa Wote; Kampeni iliyoanzishwa na Premier Projects kuboresha michezo ya kijamii ndani ya bara la Afrika. Mradi wa Michezo kwa wote utaendelea kukuzwa Pamoja na maendeleo ya Elimu kwa Wote ndani ya mwaka 2021.

Unaweza kujifunza Zaidi kuhusu Premier Projects kwenye akaunti za tovuti yao, Facebook, Instagram na YouTube.