Premier Projects imesaidia kukabili Changamoto za Kimazingira nchini Tanzania

Imechapishwa: 24 Novemba, 2020

Premier 6

Premier Projects imesaidia kupanda miti 600 nchini Tanzania, kuonyesha usaidizi wao kwenye kutunza mazingira.

Imefanikwa kutoa msaada wa kifedha kufanikisha mradi huu kwa pamoja na Habari Development Association.

Lengo la Chama ni kuelimisha jamii kuhusiana na uchumi wa jamii na maendeleo na kutunza misitu. Pia wanapambana kuyalinda mazingira kutokana na uharibifu, na pia kupanda miti ili kuepusha kuenea kwa jangwa.

Premier Bet na kikundi chao cha Hisani, Premier Projects, wameshiriki kwenye upandaji wa miti kwenye mji mkuu wa Tanzania, Dodoma. Na pia, Premier Bet walijitolea mashati ya Polo kwa jamii iliyowazunguka.

Msemaji kutoka Premier Bet Tanzania alisema: “Premier Bet, tunaamini kuyalinda mazingira ni moja kati ya changamoto kubwa zinazoikabili Dunia sasa. Kwenye jamii zetu za KiTanzania, kushindwa kuyalinda mazingira kunaweza kusababisha majanga makubwa ya kijamii.

Kusaidia Chama cha maendeleo ya Habari kwenye malengo yao kuyatunza mazingira na kuelimisha watu umuhimu wake, ni kitu kinachotupa fahari sana.”

Kufahamu Zaidi kuhusu Premier Projects na kazi zao za Hisani wanazofanya barani Afrika, watembelee kwenye kurasa zao za Facebook, Instagram na YouTube.