WAJIBU WA PREMIER BET

Premier Bet hujitahidi kuhakikisha kuwa mazingira ya kushiriki mchezo katika Premier Bet ni shwari. Kwa watu wengi, kucheza kamari kunafurahisha na kutoa burudani isiyo na madhara. Lakini, wakati mwingine hupita kiasi ambapo idadi ndogo ya wachezaji hawadiriki kuteua michezo zaidi au kuweka bet ya ziada.

KWA WENYE UMRI WA ZAIDI YA MIAKA 18 PEKEE

Nchini Tanzania ni hatia kwa yeyote aliye chini ya umri wa miaka 18 kucheza kamari. Premier Bet ina haki ya kuulizia ithibati ya umri wa mteja na kuthibitisha habari zilizotolewa.
Akaunti ya mteja inaweza kuzuiwa kwa muda na pesa kuzuiliwa hadi umri wake uthibitishwe.

JUA UPEO WAKO

Mfumo wetu katika Premier Bet unahusisha kiwango cha amana cha ulimwengu ambacho kimewekwa na idara yetu ya huduma kwa wateja. Kiwango hiki kinajisimamia kando na yale malipo yaliyowekwa na wafanyabiashara ambayo yanapatikana katika kurasa zetu za amana.

Kiwango hiki kinajumuisha:

KIWANGO CHA AMANA

• Kiwango cha amana kwa saa 24 - Unaamua kiwango cha pesa unachoweka kama amana ndani ya saa 24
• Kiwango cha amana kila wiki - Unaamua kiwango cha pesa unachoweka kama amana ndani ya wiki moja
• Kiwango cha amana kila mwezi - Unaamua kiwango cha pesa unachoweka kama amana ndani ya mwezi mmoja

KIWANGO CHA BET

• Kiwango cha Bet kwa saa 24 - Unaamua kiwango cha pesa unachowekeza kwa Bet ndani ya saa 24
• Kiwango cha Bet kila wiki - Unaamua kiwango cha pesa unachowekeza kwa Bet ndani ya wiki moja
• Kiwango cha Bet kila mwezi - Unaamua kiwango cha pesa unachowekeza kwa Bet ndani ya mwezi mmoja

KIWANGO CHA HASARA

• Kiwango cha hasara kwa saa 24 - Unaamua kiwango cha pesa unachoweza kupoteza ndani ya saa 24
• Kiwango cha hasara kila wiki - Unaamua kiwango cha pesa unachoweza kupoteza ndani ya wiki moja
• Kiwango cha hasara kila mwezi - Unaamua kiwango cha pesa unachoweza kupoteza ndani ya mwezi mmoja

Hasara na viwango vya Bet huhakikishwa kila mara unapoingia kwenye tovuti yetu. Iwapo hasara yako au bets zako zinazidi kiwango ulichoweka, hutaweza kuwekeza Bet nyingine hadi muda uliyoweka ukamilike.

KUFUATILIA MIAMALA YAKO

Unaweza kufuatilia historia ya miamala, pesa ulizotoa na kuweka kupitia kwa kitengo cha ’Akaunti Yangu’ kwa urahisi. Baki yako huonyeshwa kupitia kwa ’Akaunti Yangu’ kutoka kwa ukurasa wa kwanza wa Premier Bet. Unaweza kutazama kumbukumbu za shughuli zako za kila mwezi moja kwa moja mtandaoni. Kwa shughuli nyinginezo, tafadhali wasiliana nasi.

UFUNDISHAJI NA UHAMASISHAJI WA WAFANYAKAZI

Wakurugenzi wetu wote pamoja na wafanyakazi wa Auni kwa Wateja hupokea uhamasishaji na mafunzo kuhusu masuala ya kamari.

KUSALIA KWENYE UDHIBITI

Japo wengi wa wacheza kamari hucheza kulingana na uwezo wao, kwa wengine mchezo wa kamari huweza kuwa tatizo. Yaweza kukusaidia kuuthibiti kupitia yafuatayo:

• Mchezo wa kamari unafaa kuburudisha na wala haufai kuchukuliwa kama njia ya kujipatia riziki.
• Usicheze kufidia hasara
• Wekeza katika mchezo wa kamari kile ambacho uko radhi kupoteza
• Zingatia muda na kiasi cha pesa unazotumia katika mchezo wa kamari

Iwapo unahisi kwamba mchezo wa kamari umedhuru maisha yako au ya mwenzako, maswali yafuatayo yanaweza kukusaidia kugundua:

• Je, wewe hukosa kwenda kazini, chuoni, au shuleni kwa sababu ya kucheza kamari?
• Je, wewe hucheza kamari ili kujinasua kutoka kwa upweke au kukosa furaha?
• Unapoishiwa na pesa wakati wa kucheza kamari, je, wewe huhisi kuwa umepotoka na kutamauka na unahitaji kucheza tena haraka kadri iwezekanavyo?
• Je, wewe hutumia pesa zote kwenye mchezo huu kiasi cha kukosa nauli ya kwenda nyumbani au hata kununua kopo la chai?
• Je, umewahi kudangany’a ili kuficha kiwango cha pesa ulizotumia au wakati uliotumia kucheza kamari?
• Je, umewahi kukashifiwa kuhusiana na uchezaji kamari?
• Je, umewahi kukosa shauku kuhusu familia, marafiki au jambo ulipendalo?
• Baada ya kupoteza, je, unahisi kwamba ni lazima ujaribu tena kucheza na kushinda ili kukomboa hasara haraka kadri iwezekanavyo?
• Je, mabishano, kuvunjika moyo au masikitiko hukuchochea kucheza kamari?
• Je, unahuzunika au hata kutaka kujiua kwa sababu ya kucheza kamari?

Kadri unavyojibu ‘ndiyo’ ndivyo inavyobainika kuwa huenda una tatizo sugu la mchezo wa kamari.

KUJITENGA

Kujitenga’ ni huduma mojawapo tunayotoa kwa wale wateja wanaohisi kuwa uchezaji kamari umewapiku na wanataka tuwasaidie kujikwamua. Kwa kukubali maafikiano na Premier Bet kuhusu ‘Kujitenga’, utazuiwa kutumia akaunti yako kwa kipindi cha muda utakaoteua.

Unaweza kuteua kati ya:

• Kujitenga kwa Siku Moja
• Kujitenga kwa Wiki Moja
• Kujitenga kwa Mwezi Moja
• Kujitenga kwa Muda kwa Mujibu wa Desturi zilizowekwa
• Kufunga akaunti yako daima

Katika kipindi hiki, hutaweza kupokea matangazo au bidhaa zozote kutoka kwetu. Iwapo unataka kufunga akaunti yako daima, tafadhali wasiliana na auni yetu

wasiliana na auni yetu