BET ZA BILA MALIPO NA MASHARTI YA KIPEKEE

Mara kwa mara huenda tukatoa vichocheo, mashindano, bonus, ofa maalum na/au bets za bila malipo kwa akaunti mpya. Huwezi kupata ofa za akaunti mpya iwapo tayari wewe ni mteja aliye na akaunti.

Tuna  uhuru na haki ya kuchagua wateja waliopo tayari na kuwajumuisha katika baadhi ya vichocheo, mashindano, bonus au hata ofa maalum bila kuhitajika kutoa sababu.  Vichocheo hivi vinategemea sheria na masharti ya ziada pamoja na muda wa uhalali unaotolewa vinapotumika. Ili kupata vichocheo hivi lazima utimize sheria na masharti ya ofa husika. Iwapo utakosa kujisaljili na kuweka pesa katika muda uliotengwa au utakosa kutimiza sheria na masharti mengine yaliyotolewa, bet yako ya bila malipo/ushindi maalum itatwaliwa.

Isipokuwa pale inaelezewa vingine, bets zote za bila malipo sharti zikombolewe dhidi ya ushindi wa bet moja. Iwapo kuna mgongano baina ya sheria na masharti haya na sheria na masharti mahususi ya shindano hili, sheria na masharti mahususi ya shindano yatazingatiwa.

Sheria na Masharti ya Bonasi

KUFUNGUA AKAUNTI

Ili kuweka bet au kucheza mchezo kutumia huduma hii, utahitajika kufungua akaunti nasi (“Akaunti” yako). Kwa kufungua Akaunti na kwa kutumia huduma hii unathibitisha kwetu sote kuwa kila wakati:

(a) uko na umri wa miaka 18 au zaidi (Ni hatia kucheza kamari kama hujahitimu miaka 18 au zaidi); (b) Una uwezo kisheria wa kuingia mikataba yenye masharti; (c) uko katika himaya ambapo ni halali kufungua akaunti nasi na kutumia huduma zetu. (d) wewe ndiye unayesema ndiwe  katika usajili, unatoa taarifa sahihi na kamilifu na kwamba utatufahamisha haraka iwezekanavyo iwapo kutatokea mabadiliko yoyote; (e) unajiandikisha mwenyewe wala sio kwa niaba ya mtu mwingine. (f) hujakuwa na akaunti nasi ambayo ama tuliifunga au ikafungwa na watoaji wengine wa huduma za kucheza kamari kwa sababu ya kukiuka kanuni au mienendo inayovunja sheria; (g) hujazuiwa kwa sababu yoyote kuweka bets nasi au kutumia  huduma zetu; na (h) hujajizuia au ukazuiwa na mtu/kitu kingine  kucheza kamari. Utakapofungua Akaunti utaombwa kutupatia taarifa za kibinafsi ikiwemo jina lako na tarehe ya kuzaliwa kwako pamoja na njia ya kuwasiliana nawe na anwani ya barua pepe.

Una wajibu wa kuhakikisha kwamba taarifa sahihi za kifedha pamoja na taarifa za kibinafsi zinapatikana katika Akaunti yako uliyofungua nasi. Kwa kutuwasilishia taarifa zako kuhusu malipo unaidhinisha kwamba wewe ndiwe unayestahiki kuedesha shughuli husika au kuweka bet kwa kutumia taarifa hizo za malipo. Iwapo hatutapokea kibali cha kufanya malipo au iwapo malipo yamebatilishwa, hayawezi kuchakatwa au iwapo kibali kitabatilishwa, huenda tukakataa shughuli yako au bet yako na/au tukafunga  Akaunti yako kabisa au tukaizuia kwa muda.

Unaweza kufungua Akaunti moja tu nasi ambayo inaweza kutumika nawe tu kwa minajili ya Huduma zetu. Tuna haki na uhuru wa kufunga Akaunti rudufu na kukatisha bets au miamala yoyote katika Akaunti hizo. Aidha, tuna haki ya kuzuia kwa muda au kufunga kabisa Akaunti yoyote pamoja na kubatilisha bets zozote zinazohusika na shughuli nyingine katika Akaunti husika iwapo mwenye akaunti na mfadhili wa bets si mtu mmoja.

USALAMA WA AKAUNTI

Tunakushauri kuhakikisha unatengeneza neno siri lako kwa umakini. Dondoo nyingine za kuhakikisha akaunti yako inakua salama:
- Mara zote hakikisha unatumia neno siri imara lenye mchanganyiko wa namba na herufi.
- Hifadhi neno siri lako kwenye simu au kifaa unachotumia wewe PEKEE.
- Badilisha neno siri lako mara kwa mara na epuka kutumia neno siri lile lile la zamani.
- Usimtajie mtu yeyote neno siri lako.
- Unapotumia kompyuta ya umma, usihifadhi neno siri lako na hakikisha una sign out baada ya kumaliza kutumia ili kuzuia watu wengine kuweza kuingia kwenye kupata akaunti yako.

Iwapo utachagua au ukapewa nywila au taarifa nyingine yoyote kama sehemu ya hatua zetu za kuhakikisha usalama wa akaunti yako, lazima uweke taarifa hizo kwa usiri na usimwambie mtu mwingine yeyote.

Utunzaji wa usiri wa nywila yako ni wajibu wako binafsi na  unatarajiwa kuwajibikia shughuli zote zinazoendeshwa chini ya jina la akaunti yako na nywila husika. Jina lolote la akaunti au nywila utakayochagua au kupewa kukuwezesha kupata Huduma zetu ni kwa matumizi yako binafsi pekee na haiwezi kuhamishika kwa mtu mwingine. Tunapendekeza uzime kumbukumbu ya moja kwa moja ya nywila katika mtandao kabla ya kuingia kwenye Tovuti. Hii itasaidia kupunguza hatari ya Akaunti yako kutumika bila kibali chako.

Unakubali:

(a) kutujulisha mara moja iwapo jina la akaunti yako na/au nywila yako itatumika bila kibali chako au  uvunjaji mwingine wowote wa usalama wa akaunti yako; na (b) kuhakikisha kwamba unatoka kwenye Akaunti yako unapokamilisha shughuli zako. Hatuwezi na hatutakubali kuwajibikia kisheria hasara au madhara yoyote yatakayotokana na kutotimiza mahitaji katika masharti haya.

Iwapo utasahau jina la Akaunti au nywila yako tafadhali wasiliana nasi mara moja. Tutatumia mbinu zote halali na ziwezekanazo kuzuia kwa muda matumizi ya Akaunti yako punde tu unapotufahamisha kupotea kwa taarifa za uslama wa Akaunti yako. Hata hivyo utasalia kuwajibikia bets zote zilizowekwa katika akaunti yako kabla ya kuzuia matumizi ya Akaunti husika. Iwapo tuna sababu za kutufanya kuamini kwamba kuna uwezekano wa kuvunja usalama au matumizi mabaya ya Akaunti yako, huenda tukakuhitaji kubadilisha nywila au taarifa za usajili au tukazuia kwa muda ama hata kufungua Akaunti yako bila kutoa ilani.

Tuna haki ya kuzima, kuzuia kwa muda au kudhibiti jina la Akaunti au nywila, iwe uliichagua au tulikupatia wakati wowote kwa hiari yetu iwapo kwa maoni yetu umeshindwa kufuata maagizo katika Makubaliano haya.

Huenda usiweze:

(a) kuweka, kuchagua au kutumia jina bandia, anwani, taarifa za Akaunti au anwani ya barua pepe inayomilikiwa au kusimamiwa na mtu mwingine kwa nia ya kujifanya kuwa mtu huyo, au (b) kutumia jina au taarifa kama hizo bila ya kibali faafu. Hatutakubali kuwajibikia kisheria hasara yoyote itakayotokana na matumizi yasiyoidhinishwa ya Tovuti yetu na/au Huduma zetu, iwe ni kwa njia  ya udanganyifu au vinginevyo. Tuna haki ya kukataa usajili kwa hiari yetu, au kuzuia kwa muda au kubatilisha jina la akaunti bila ya kutoa notisi.

HATARI

Unakubali na kuthibitisha kwamba unafahamu kwa ukamilifu kuwa kuna hatari ya kupoteza pesa unapocheza kamari kupitia kwa Tovuti yetu na/au Huduma zetu na kwamba unawajibikia kikamilifu hasara kama hizo.

SHUGHULI KATIKA KAUNTI YAKO

IIli kushiriki katika kuweka bet  au huduma nyingine, sharti kwanza uweke pesa katika Akaunti yako. Baada ya Akaunti yako kufunguliwa, unaweza kuweka pesa kupitia kwa njia mbalimbali. Tunakubali malipo kupitia kwa huduma za malipo kwa simu za mkononi zilizoonyeshwa kwenye Tovuti yetu na kwa kutumia vocha zetu. Tuna haki ya kubadilisha njia za kuweka pesa tunazokubali mara kwa mara.

Tuna haki ya kuzuia pesa pale ambapo tuna sababu za kutosha kutufanya kuamini kwamba mtumiaji wa akaunti na mwenye Akaunti ni watu tofauti (na ushindi wowote unaotokana na pesa zilizowekwa kwa njia hii utabatilishwa).

Tuna haki, kwa hiari yetu na bila ya kuhitajika kutoa sababu, ya kukataa kupokea malipo yanayowasilishwa kwetu hata kama awali tulikubali malipo kama hayo kutoka kwako au hata kama kwa kawaida tungepokea malipo kama hayo kutoka kwa mteja yeyote.

Hatulipizi kuweka au kutoa pesa lakini unafaa kuchunguza na benki yako na/au wanaosimamia mifumo mingine ya kutoa huduma za kufanya malipo iwapo watakulipisha ada yoyote kwa huduma zao.

Vifaa vya Akaunti zinatolewa kwako kwa lengo la kukuwezesha kuweka bets au kushiriki katika Huduma zetu pekee. Iwapo utaonekana kuweka na kutoa pesa, kwa sababu yoyote ile, bila kushiriki michezo yetu kwa uaminifu, tuna haki ya kutoza gharama zozote tulizopata kwa Akaunti yako bila ya kutoa ilani kabla ya kuifunga. Hali hii huenda ikaishia kwa kutoa ripoti kwa vyombo vya usalama na Akaunti kuzuiwa kwa muda au kufungwa.

Salio utakaloweka kwenye akaunti yako litatakiwa kuzungushwa kiasi chote, angalau mara moja kwenye matokeo ambayo hayajasuluhishwa kwa 1.00 au kurudishiwa salio katika kitabu cha michezo.

Kuambatana na mahitaji ya sheria za nchi yako kuhusu ushuru, una jukumu la kuripoti pesa unazoshinda au kupoteza kupitia kwa Huduma hizi.

Salio katika Akaunti halizai riba. Ukopaji hauruhusiwi. Ni jukumu lako kuhakikisha kuna pesa za kutosha katika Akaunti yako na kuweka bets zako inavyopasa. Tuna haki ya kubatilisha bet yoyote au shughuli nyingine ambayo huenda tuliichakata kwa kughafilika iwapo Akaunti yako haina pesa za kutosha kusimamia shughuli husika  kikamilifu na/au kurejesha kiasi chochote kilichopunguka.

Pesa zinaweza kutolewa katika Akaunti yako mradi:

(a) malipo yote yaliyofanywa katika Akaunti yako yameidhinishwa kuwa yameandikishwa na hayajakwama, kugeuzwa au hata kubatilishwa; (b) uthibitishaji wowote wa utambuaji tunaohitajika kufanya kuambatana na sheria zinazozuia utakatishaji wa fedha unakamilika kama inavyohitajika. Kuambatana na haya, tuna haki ya kutafuta taarifa za ziada kadri tutakavyohitaji ili kuthibitisha utambulisho wako na kwa mujibu wa Sheria na Masharti haya na sheria nyingine husika;
(c) umetimiza Sheria naashaMrti haya; ;
(d)  umethibitishwa kuwa na umri wa miaka 18 na zaidi;

Inapotokea hujaweza kufanya malipo yako kwa njia unayopendelea, kikosi chetu cha Hufduma kwa Wateja kitawasiliana nawe na kupanga njia mbadala wa kufanya malipo Tafadhali zingatia kuwa njia ya kutoa pesa lazima ifanane na njia uliyotumia mwisho kuweka pesa.

MAKOSA

Hatutakubali kuwajibikia kisheria makosa yoyote yanayohusu kutangaza, kuchapisha au kuweka bei, handicap, masharti ya bet, taarifa kuhusu bet au matokeo licha ya juhudi zetu kuhakikisha usahihi. Tunafanya kila juhudi kuhakikisha kwamba makosa yanayofanywa kuhusu bei zilizotolewa au bets yanakubaliwa. Hata hivyo kosa la kibinadamu na/au la programu wakati mwingine huenda likazalisha makosa. Tuna haki ya kufanya marekebisho kwa makosa ya wazi na ya kubatilisha bets zilizowekwa ambapo makosa haya yametokea. Iwapo kuna makosa ya wazi katika bei zilizotolewa (ikiwemo kwa mfano tukio ambapo bei inayoonyeshwa ni tofauti na iliyopo katika maduka ya mengine na/au bei husika inadhihirika wazi kuwa si sahihi kutegema hali zote), bets zitalipwa kwa kutumia bei sahihi wakati wa kukubaliwa. Iwapo tunaikubali bet kwa shindano ambapo kutoa bei kwa shindano husika (badala ya bei yenyewe) ilikuwa makosa, bet husika itabatilishwa na pesa zako kurejeshwa katika akaunti yako.

Iwapo pesa zitawekwa katika Akaunti ya mteja kimakosa, ni jukumu la mteja husika kutufahamisha kuhusu kosa hilo bila kukawia. Ushindi wowote unaotokana na kosa husika na kabla ya kutufahamisha, iwe unahusishwa na kosa lenyewe au la, utafutiliwa mbali na kurudishwa au  vinginevyo tunaweza kukudai.

MIGOGORO YA  BETTING

Maswali yoyote kuhusu bet yanapaswa kutumwa kwetu kwanza kupitia kwa barua pepe. Tutafanya kila juhudi kutatua suala husika kwa njia inayokubalika kwa pande zote mbili.

KUWEKA BETS ZAKO

Lazima ufanye uamuzi wako katika kuchagua bet utakayoweka. Unakiri kuwa kwa kuweka bet yako, hutegemei yaliyosemwa na mfanyakazi wetu yeyote kuhusu bet husika. Tuna haki ya kukataa bet yote au sehemu ya bet  yoyote.

Unakubali kutulipa kwa bets unazoweka nasi kwa mujibu wa Sheria na Masharti. Unakubali kuwa unawajibikia bets zote ulizoweka katika Akaunti yako uliyofungua nasi. Bets kwenye tovuti yetu zinaweza kuwekwa nawe tu kupitia kwa Akaunti yako na hatutakubali bets kutoka kwako kupitia kwa njia nyingine au mfumo mwingine kuhusiana na Huduma hizi. Ushindi wowote kutokana na matumizi ya tovuti au huduma zetu utawekwa katika Akaunti yako na bets zitakazofuata zitatolewa kutoka kwa salio kwenye Akaunti yako nasi.

Wateja wanaweza kuweka bets; zenye thamani ya pesa katika Akaunti zao au zisizovuka kiwango kilichowekwa katika sheria za kuweka bets, yoyote iliyo na thamani ya chini. Sisi tu ndio tunaoamua kiwango cha juu na cha chini cha bet kwa kila chaguzi. Ili kuweka bet au kupata Huduma, fuata,maagizo yaliyotolewa kwenye sehemu ya Msaada katika Tovuti

Ni jukumu lako kuhakikisha kwamba bet yoyote au shughuli yoyote unayoweka kwa kutumia Huduma zetu ni sahihi.

Tuna haki ya kukataa shughuli nzima au sehemu ya shughuli uliyoomba wakati wowote tunapoamua au wakati ambapo umekiuka Sheria na Masharti. Hakuna shughuli tunayokubali hadi unapotoa thibitisho faafu (au vinginevyo tunapoikubali).

Baada ya kuweka bet na umepokea thibitisho kuwa bet yako imekubalika huwezi kuifuta (isipokuwa pale ambapo sisi, kwa uamuzi wetu, tunatoa kibali kuifuta au kuibadilisha bet). Katika hali hiyo umetupatia kibali ambacho hakiwezi kufutiliwa mbali kushika pesa zako tukisubiri matokeo ya shindano husika na ama kutwaa, kurejesha au kulipa pesa ulizoshinda kwa mujibu wa bet yako na kuambatana na kanuni za kucheza kamari zinazoongoza bet husika na kwa mujibu wa Sheria na Masharti haya.

Wakati bets zinawekwa baada ya shindano kuanza,  zitasalia kuwa halali iwapo hakuna tukio lililotokea ambalo linaathiri nafasi za uteuzi husika kushinda au kushindwa. Bets zote zitakazowekwa baada ya matokeo ya shindano kujulikana zitabatilishwa (iwe zimeshinda au kushindwa). Tuna haki ya kubatilisha bet  zilizokubalika kibahati mbaya baada ya kipindi cha kuweka bets kufungwa au wakati ambapo mchezo ulikuwa umekamilika au katika kiwango ambapo mteja angekuwa amepata  ishara za matokeo ya mechi. Tuna haki zaidi ya kubatilisha bet yoyote  baada ya tukiohusika kuanza. Hali hii itatumika hata kama tumetangaza wakati wa kuanza kimakosa au umetangazwa kimakosa na vyombo vya habari kwingineko.

Iwapo kutatokea mtafaruku kuhusu ni wakati gani bet iliwekwa au iwapo bet imewekwa, basi wakati ambapo ilirekodiwa (iwapo ilirekodiwa) kwenye  usajili wetu ndio utakaorejelewa katika kutatua mtafaruku husika. Iwapo jaribio la kuweka bet halikurekodiwa katika sajili yetu ya shughuli basi itachukuliwa kwamba hakuna bet iliyowekwa. Unapaswa kuangalia salio katika Akaunti yako kila mara unapoingia kwenye Tovuti yetu.

Tafadhali jifahamishe kwa istilahi na misamiati maalum ya kucheza kamari na jinsi bets mbalimbali na michezo inaendeshwa. Iwapo una maswali yoyote kuhusiana na hali hizi tafadhali wasiliana nasi. Hatutakubali kuwajibikia hali  ambapo umeweka bet bila kuelewa vizuri sheria na masharti yanayohusika au jinsi bet husika au mchezo unaendeshwa.

Katika hali ambapo mawasilisho uliyofanya yanathibitishwa kuwa ya uwongo, pesa ulizoweka zitatwaliwa na hatutahitajika kukulipa ushindi wowote ambao huenda tungekulipa kwa minajili ya bet husika. Maswali yoyote kuhusu bet uliyoweka kwenye tovuti sharti uyaulize mwenyewe katika muda usiozidi miezi sita baada ya mechi ya mwisho katika bet yako imekamilika. Hatuwezi kukuahidi kuwa tutashughulikia swali lako iwapo halitaulizwa katika kipindi hiki.

Kima cha juu cha ushindi kwa kila bashiri ni 500,000,000 TSH. Bashiri yoyote yenye alama sare na machaguo sare yanachangia kwenye kima cha juu cha ushindi.

ULAGHAI & BETS ZILIZOBATILISHWA

Tuna haki ya  kutafuta adhabu za jinai au adhabu nyinginezo dhidi yako iwapo tutashuku kuwa umehusika katika ulaghai, hujawa mwaminifu au umefanya makosa ya jinai na tukatoa taarifa kama hizo kwa mamlaka husika au kwa wenzi wetu kutoka nje (kama vile watoaji huduma za kufanya malipo) kama hali itakavyohitaji.

Kima cha juu cha ushindi (maximum payout) kwa kila mteja ndani ya siku pia ni 500,000,000 TSH.

Tuna haki ya kuzuia kwa muda au kufunga Akaunti yoyote ambayo tunaamini inahusika katika ulaghai, utakatishaji wa fedha na/au mienendo mingine inayokiuka sheria au inayotiliwa shaka. Aidha tuna haki ya kuripoti taarifa kama hizi kadri tunapochunguza tukio kwa mamlaka faafu.

Tuna haki ya kusimamisha malipo kwako pale ambapo unashukiwa kuhusika katika ulaghai, kutokuwa mwaminifu au kuhusika katika shughuli za jinai.

Utatuondolea lawama na utahitajika kutulipa, tunapodai, gharama zote , hasara au kesi tutakazoingia (Ikiwemo hasara za moja kwa moja au za kiuhusisho, ikiwemo hasara katika faida au kampuni kuharibiwa jina) zinazohusika moja kwa moja au zinazohusishwa na ulaghai wako, kukosa uaminifu au makosa ya jinai.

Tuna haki ya kukataza malipo  kwa bet yoyote ambayo tunashindwa kuthibitisha kutoka kwa rekodi zetu za usalama. Tuna haki ya kubatilisha bet yoyote ambayo tunaamini si halali au inayokiuka Sheria na Masharti haya, sheria yetu yoyote kuhusu uwekaji bets au sheria zozote za shirika la kusimamia  uchezaji kamari.

Tuna haki ya kukataza au kudhibiti bets zozote kwa hiari yetu kwa sababu yoyote ile. Katika hali ambapo bet inachukuliwa au inathibitishwa kuwa imebatilishwa nasi kwa hiari yetu, pesa zozote zilizokatwa kwenye Akaunti yako kwa ajili ya bet husika zitarejeshwa kwenye Akaunti yako. Bets zitakuwa halali iwapo tu zimekubalika na mitambo yetu. Hadi zikubalike, hakuna mawasiliano kutoka kwako ambayo yatatufunga kisheria na taarifa zote zinazoonyeshwa kwenye tovuti zinajumuisha  mwaliko  wa kutoa Huduma pekee. Iwapo tutaamua kuondoa sheria fulani ili kuhakikisha  tunakutendea haki, itakuwa ni kwa mchezo huo pekee na haitakuwa kigezo cha kurejelea siku zijazo.

KUZUIA AKAUNTI KWA MUDA

Hatuahidi, kuhakikisha au kueleza kuwa Huduma zote zitatolewa kwa wateja wote. Huenda kwa hiari yetu na bila kuhitajika kutoa sababu tukawaondoa baadhi ya wateja kutoka kwa  Huduma zetu kabisa au kuwazuia kushiriki baadhi ya mashindano na ofa tutakazotoa mara kwa mara. Bila kudhibiti uwezo wetu wa kutegemea hatua nyingine za kurekebisha zilizopo, huenda tukazuia kwa muda au tukafunga Akaunti yako, kuzuia sehemu ya salio au salio lote kwenye Akaunti au kubatilisha bets na shughuli ulizoweka kwa hiari yetu wenyewe iwapo:

(a) Kuna tatizo la teknolojia linaloathiri maadili ya shughuli au Akaunti yako; (b) Tunashuku au tunajua kuwa unahusika katika shughuli zinazokiuka sheria au za ulaghai utapotumia Huduma zetu;  (c) Tunashuku au tunajua kuwa umekiuka sehemu yoyote ya Sheria na Masharti haya au sheria zinazodhibiti bet au shughuli fulani; (d) Tunashuku au tunajua kuwa una mienendo ambayo inaweza  kuleta madhara kwa namna tunayoendesha biashara yetu au vinginevyo unaendesha shughuli kwa njia isiyo ya haki kwetu au kwa mchezaji mwingine kwa  kutumia  dosari, mwanya au tatizo kwenye programu yetu au kwa kudanganya na kupanga njama na wengine; (e) Tunashuku au tunajua kuwa huenda unapata ugumu kupata pesa, umefilisika au ukawa umepitia hatua kama hizi popote ulimwenguni; (f) Kwa uamuzi wetu kuna kosa linalojitokeza kuhusiana na bet uliyoweka au shughuli uliyohusika; (g) Tutapata kujua kuwa umegeuza au kukataza bets au shughuli za kuweka pesa ulizofanya katika Akaunti yako; au (h) Sheria inatuhitaji kufanya vile.

KUFUNGWA KWA AKAUNTI

Tafadhali wasiliana nasi iwapo unataka kufunga Akaunti yako. Tutashughulikia ombi lako katika kipindi chenye maana, lakini utaendelea kuwajibikia shughuli zote katika Akaunti yako hadi pale Akaunti hii itafungwa rasmi(yaani, bets zote zilizowekwa na shughuli nyingine ziwe zimetimizwa na pesa zote kwenye Akaunti kulipwa au kutolewa kwa mujibu wa Sheria na Masharti yetu)

Tuna haki ya kufunga Akaunti kwa hiari yetu na bila kuhitajika kutoa sababu  zozote kupitia kwa notisi iliyoandikwa ( au notisi iliyojaribiwa) kwako kupitia kwa taarifa za mawasiliano uliyotupatia. Salio lolote katika Akaunti yako ambalo halina ukinzani litatolewa kwako mradi utazingatia Sheria na Masharti.

Huenda pia tukafunga Akaunti yako au kuizuia kwa muda iwapo Akaunti itabaki bila kutumiwa kwa kipindi kirefu.  Iwapo hautatumia Akaunti yako kuweka bet au kushiriki michezo, kuweka pesa au kutoa ama  iwapo Akaunti yako itakuwa haitumiki kwa kipindi cha angalau miezi 24 mfululizo basi itafungwa na urejeshewe salio ambalo halina ukinzani.

Katika hali ambapo tumeifunga Akaunti yako kwa sababu yoyote ile, hahutawajibika kwako tena zaidi ya kurejesha salio lolote ambalo halina ukinzani.

Tunapofunga Akaunti yako kutokana na ukiukaji wa Sheria na Masharti yetu, salio katika Akaunti yako halitarejeshwa na litachukuliwa kuwa umelipoteza kuambatana na madai yoyote ambayo huenda tukawa nayo dhidi yako kufikia taehere ya kufungwa kwa akaunti (iwe chini ya Akaunti yako au vinginevyo). Tuna haki  ya kujilipa kutoka kwa Akaunti yako kufikia kiwango ambacho kitafidia hasara yoyote, uharibifu, gharama, matumizi au  dhima inayotokana na ukiukaji wako.

Ufungaji wa Akaunti vinginevyo hautaathiri bets zozote ambazo zimewekwa na hazijakamilika, mradi bets kama hizo bado ni halali  na haujakiuka Sheria na Masharti kwa njia yoyote ile. Akaunti yako inapofungwa au ukatoa notisi ya kufunga Akaunti yako, mashindano yoyote ambayo hayajadaiwa, bonasi au ruzuku nyingine ambazo zilikuwa zimetolewa kwako zitabatilishwa  moja kwa moja.

Makubaliano haya yanapovunjwa, ama nasi au nawe, unakubali na kukiri kwamba:

(a) Haki yako ya kutumia Tovuti na huduma zetu itasitishwa mara moja     (b) Utasitisha matumizi yote ya Tovuti na Huduma zetu, na (c) Utaondoa programu ulizopewa au ulizopakua zinazofungamana na Tovuti yetu kutoka kwa tarakilishi, kipakatalishi au kumbukumbu za tarakilishi pamoja na kwenye mitandao au hifadhi nyingine.

MATUMIZI KUBALIFU YA TOVUTI NA HUDUMA ZETU

Lazima uhakikishe kwamba hautumii Tovuti na/au Huduma zetu vibaya kimakusudi au kutokana na  ukosefu wa umakinifu wako ukaweka virusilishi na programu nyingine zenye madhara ya kiteknolojia. Sharti uepuke kujaribu kuingia kwenye Tovuti na/ au Huduma zetu bila kibali, sava ambapo tovuti na huduma zetu zinahifadhiwa au tarakilishi au kanzidata zozote zinazofungamana na Tovuti na Huduma zetu. Lazima uepuke kushambulia Tovuti yetu kupitia kwa shambulizi la kuzuia utoaji huduma au  usambazaji wa uzuiaji wa utoaji wa huduma. Kwa kufanya mashambulizi haya utakuwa umefanya kosa la jinai. Huenda tukaripoti mashambulizi kama haya kwa mamlaka husika na tutashirikiana na mamlaka hayo kwa kutoa utambulisho wako na taarifa nyinginezo zinazohusiana na Akaunti uliyofungua nasi. Unapokiuka masharti ya matumizi ya tovuti yetu, haki yako ya kuitumia Tovuti na Huduma zetu inasitishwa mara moja.

Shughuli zifuatazo zimejumuishwa katika “Mienendo Iliyozuiwa” na ambazo haziruhusiwi na zitachukuliwa kama ukiukaji wa Sheria na Masharti yetu. Tutafanya kila juhudi kuzuia na kutambua mienendo kama hii na kutambua wahusika iwapo ukiukaji utatokea. Kuambatana na yoliomo hapo chini, hatutawajibikia hasara au uharibifu wowote ambao huenda ukatokea kutokana na Mienendo Iliyozuiwa na hatua zozote tutakazochukua  kufuatia hayo zitakuwa kwa hiari yetu wenyewe. Mienendo Iliyozuiwa kuambatana na Huduma zetu:

(a) matumizi mabaya ya bonasi au mashindano mengine; na/au (b) kutumia vipengele vya nje au athari ( kwa kawaida tunaita udanganyifu); na/au kujipa faida kwa njia isiyo ya haki; (c) kufungua akaunti rudufu; na/au (d) kufanya ulaghai au kushiriki vitendo vya jinai.

Hatuna jukumu la kuchunguza au kusimamia shughuli au matumizi ya Tovuti ya mteja yeyote. Hata hivyo tuna haki wakati wowote ya kuchunguza, kuweka na kutoa taarifa zozote kama inavyohitajika kutimiza mahitaji ya sheria husika, udhibiti, mchakato wa kisheria au ombi kutoka kwa mamlaka ya udhibiti ili kuhakikisha kuwa huduma zetu zinatumika ipasavyo, kwamba Sheria na Masharti haya yanazingatiwa au ili kuchunguza ukiukaji tunaoshuku.

HAKI MILIKI

Unakubali na kukiri kwamba haki miliki katika Tovuti yetu, yaliyomo (ikiwemo programu yoyote) na yaliyochapishwa kwenye tovuti inasalia wakati wote kwetu au kwa watoaji leseni. Haki hizi zinajumuisha, bila kujifungwa kwa, hakimiliki, alama za biashara, programu zinazoendesha tovuti, usanifu, picha, mpangilio, mtazamo,  hisi na muundo wa Tovuti yetu, haki za higfadhidata, haki za usanifu, majina ya uwanja na haki za  ukarimu na/au sheria za alama za biashara ambazo hazijasajiliwa. Unaweza kuruhusiwa kutumia  nyenzo na yaliyomo kama inavyoidhinishwa na watoaji wa leseni. Unakubali na kukiri kuwa nyenzo na yaliyomo katika Tovuti yetu yametolewa kwako kwa minajili ya matumizi ya kibinafsi na yasiyo ya kibiashara pekee. Matumizi yoyote mengine ya nyenzo na yaliyomo ni marufuku. Unakubali (na unakubali kutosaidia mtu au asasi yoyote)   kutonakili, kutorudufu, kutopeperusha, kutochapisha, kutosambaza, kutotumia kibiashara,badilisha au kubuni kwa kuiga nyenzo na yaliyomo.

Hatutoi kibali chochote kwako moja kwa moja au kifahamivu kuhusu haki miliki za tovuti au taarifa za siri.

Ili kuondoa tashwishi, unaweza kutumia data iliyopo kwenye Tovuti (ikiwemo kwa mfano odds, za moja kwa moja au za kihistoria) kama inavyohitajika kwa mujibu wa kibali cha kibinafsi, kwa dhima isiyo ya kibiashara ya kutoa Huduma hizi. Matumizi mengine yoyote na/au urudufu wa data bila kibali chetu ni marufuku na yatachukuliwa kuwa ukiukaji wa Sheria na Masharti yetu. Tuna haki ya kuchukua hatua yoyote tutakayoona inafaa, ikiwemo kuanzisha mashtaka bila ya kutoa notisi kwako kwa kurejelea matumizi yoyote yasiyoruhusiwa ya data kwenye tovuti au Tovuti yenyewe.

HAKI ZA WATU NA ASASI NYINGINE

Isipokuwa pale inapoelezwa wazi wazi, hakuna kipengele chochote kwenye Sheria na Masharti kitakachojenga au kutoa haki au manufaa mengine yoyote kwa mtu mwingine yeyote kando na wewe na sisi.

UDONDOSHAJI

Iwapo Sheria na Masharti yoyote yatabainishwa na asasi yenye mamlaka kuwa yasiyo na mashiko,, kinyume na sheria, batili au yasiyoweza kutekelezwa kwa kiwango chochote, sheria au masharti husika yatadondoshwa kutoka kwa sheria na masharti yanayosalia ambayo yataendelea kuzingatiwa kwa kiwango kinachowezeshwa na sheria.

DATA YA KIBINAFSI.

Tunachakata na kuhifadhi  taarifa za kibinafsi kuambatana na Sera yetu ya Faragha na Sera ya Vidakuzi.

Tunahitajika kutoa taarifa za kibinafsi tulizonazo kukuhusu zinazojumuisha data ya kibinafsi na historia yako ya kuweka bets kwa msimamizi, asasi za uchezaji kamari na asasi nyinginezo ikiwemo polisi ili kuwezesha uchunguzi wa ulaghai, utakatishaji wa fedha au masuala ya maadili katika michezo pamoja na kutimiza majukumu yetu ya udhibiti.

DHIMA NA  FIDIA

Umekubali kuwa kutumia tovuti yetu ni juu yako mwenyewe.

Wajibu wetu kwako kisheria unaotokana na Sheria na Masharti yetu, iwe ni kwa kukiuka mkataba, uvunjaji wa sheria (ikiwemo ukosefu wa umakini) au hali nyinginezo utajikita kwa:

(a) Kiasi cha bet husika ambapo dhima rejelewa imeibukia; na (b) Wakati ambapo tumepoteza pesa ulizoweka kwenye Akaunti yako, kurejesha kiasi sawa kwenye Akaunti yako.

Hatutawajibika kwako kisheria katika mkataba, uvunjaji wa sheria (ikiwemo ukosefu wa umakini), ukiukaji wa wajibu wa kisheria au  vinginevyo kutokana na :

(a) mchachawizo wa biashara, kupungua kwa faida, mapato, biashara, data, fursa, taarifa za kibiashara au ukarimu; au (b) hasara zisizo za moja kwa moja au hasara inayoandamana na , inayotokana na au inayohusiana na sheria na masharti haya, hata pale ambapo hasara kama hizo zimetabiriwa au iwapo umetufahamisha kuhusu uwezekano wa hasara kama hizo.

MTANDAO KUTOFANYA KAZI

Licha ya kuwa tunajitolea kuhakikisha kwamba Tovuti yetu inaweza kutumiwa bila tatizo lolote, hatutawajibikia kisheria kukawia kwake, kutotenda au kufeli kwetu ambako kutatokana na hali ambayo imevuka mipaka yetu ya udhibiti, ikiwemo  hali tusizokusudia zinazotufanya kukiuka mkataba kama vile matengenezo ya dharura, kufeli kwa mtandao, kufeli kwa kompyuta au vifaa vyake, kufeli kwa vyombo vya teknolojia ya mawasiliano au vyombo vingine, kukosekana kwa nguvu za umeme, moto, radi, milipuko, vita, mafuriko, mizozo ya kibiashara, hujuma, hali mbaya ya hewa au  vitendo vya Serikali za ugatuzi au serikali kuu au mamlaka nyingine.

Hatutawajibika kwako kisheria kwa bet ambayo haikuwekwa kwa sababu yoyote ile au wewe kukatiziwa huduma zetu, ikiwemo bila kujibana kwa, kuharibika au kukatizwa kwa unganisho la tarakilishi, huduma za mawasiliano, mtandao au vinginevyo na salio la Akaunti yako wakati wowote ule litakuwa jinsi lilivyorekodiwa katika sava zetu. Salio kwenye sava unapoingia kwenye Tovuti yetu, baada ya kukatiziwa kwa huduma, litakuwa ni kiasi baada ya kukamilisha bet yako ya mwisho kabla ya kukatiwa huduma.

SHERIA  ZINAZOTUDHIBITI

Sheria na Masharti haya yatadhibitiwa na kutekelezwa kwa mujibu wa sheria za Uganda. Unakubali bila kubatilisha kuwa mahakama za  Uganda zitakuwa na mamlaka ya kipekee ya kutatua mizozo au madai yoyote yatakayotokana na au yanayohusiana na matumizi ya Huduma zetu na kwamba sheria za Uganda zitatumika kutatua mzozo na madai  kama hayo. Hata hivyo, tuna haki ya kuanzisha mchakato wa kisheria katika himaya yoyote ambapo tunaamini kwamba ukiukaji wa haki miliki au ukiukaji wa Sheria na Masharti haya unatokea au unaanzia. Unatarajiwa kuwajibika na kufuata sheria na kanuni husika za himaya ambapo unaingia katika mtandao wetu au kutumia Huduma zetu.

MKATABA MZIMA

Sheria na Masharti haya pamoja na nyaraka iliyorejelewa humu ndani yanawakilisha mkataba mzima baina yetu nawe na yana mamlaka kuliko mikataba mingine tuliyoingia nawe hapo awali, maelewano au makubaliano baina yetu iwe kimaandishi au kwa njia ya usemi. Sote tunakiri kwamba hakuna anayenufaika na uwasilishaji, dhamana au ahadi zinazotolewa na mwingine au zilizodokezwa kutokana na chochote kilichosemwa au kuandikwa katika mawasiliano baina yetu isipokuwa kwa mujibu wa yaliyomo katika Sheria na Masharti haya.

Hakuna yeyote ambaye atafidiwa kutokana na kauli zisizo za kweli zinazotolewa na mwenzake iwe kimaandishi au kiusemi kabla ya tarehe ya mkataba (isipokuwa pale ambapo kauli kama hizo zilifanywa kwa ulaghai) na suluhu kwa muhusika wa  pili litakuwa kwa kukiuka mkataba kama ilivyoelezwa katika Sheria na Masharti .

UHAMISHO NA WAJIBU

Katika harakati za kutoa huduma kwako na kwa kurejelea matumizi ya Tovuti yetu, huenda tukahitaji kuwasiliana nawe kupitia kwa barua pepe au njia nyingine ya mawasiliano utakayokuwa umetoa kwetu. Unakubali kupokea barua pepe zetu ambazo zinalenga Akaunti yako na ambazo ni muhimu katika kuendesha Tovuti kwa njia sawa ikiwemo barua pepe ambazo zinawafahamisha wateja kuhusu matumizi ya tovuti. Unakubali kuwa tunaweza kuwasiliana nawe kuhusu Tovuti yetu kupitia kwa njia yoyote ya kielektroniki kwa simu yako au rununu.

MAWASILIANO

Licha ya kuwa matangazo ya mauzo yatadhibitiwa na Sera yetu ya Faragha na Sera ya Vidakuzi, huenda tukahitajika kuwasiliana nawe katika harakati za kutoa Huduma kwako au kuhusu matumizi yako ya tovuti yetu kupitia kwa barua pepe au kupitia kwa njia nyignine ya mawasiliano utakayokuwa umetoa kwetu. Unakubali kupokea barua pepe zetu ambazo zinalenga Akaunti yako na ambazo ni muhimu katika kuendesha Tovuti kwa njia sawa ikiwemo barua pepe ambazo zinawafahamisha wateja kuhusu matumizi ya Tovuti.

UTANGAZAJI

Kwa kushiriki katika michezo yoyote katika tovuti yetu unakubali kwamba iwapo utashinda zawadi yoyote, utaturuhusu kutumia jina lako na picha yako katika mashindano husika au kwenye vyombo vya habari bila kukuomba kibali tena au kukulipa.

VIUNGO KUTOKA KWA TOVUTI YETU

Viungo na zana kutoka tovuti nyingine zinapotolewa kwenye tovuti yetu ni kwa  ajili ya kukufahamisha pekee. Hatuna  udhibiti wa yaliyomo katika tovuti na zana hizi na hatukubali kuziwajibikia kisheria  au kuwajibikia hasara au uharibifu wowote ambao unaweza kutokea kutokana na matumizi yake, au kutokana na taarifa ambazo huenda wakapata kukuhusu (ikiwemo taarifa za kibinafsi).

Kiungo kupatikana kwenye Tovuti yetu sio idhinisho kutoka kwetu kwa matumizi ya kiungo husika, kampuni au asasi inayohusishwa na kiungo husika au yaliyomo katika tovuti inayofikiwa kwa kiungo hicho.

MABADILIKO KWA SHERIA NA MASHARTI HAYA

Tuna haki ya kubadilisha Sheria na Masharti haya wakati wowote. Tutafanya juhudi za haja kuhakikisha kuwa unapewa notisi kuhusu mabadiliko yoyote makuu kwa Sheria na Masharti haya  kupitia kwa njia faafu (kwa mfano: barua pepe au kupitia kwa notisi kwenye tovuti yetu). Hata hivyo, ni wajibu wako kuangalia Sheria na Masharti haya mara kwa mara, na kuendelea kutumia Tovuti yetu kutachukuliwa kuwa kukubali mabadiliko yoyote ambayo huenda tukafanya.

Huenda tukahitajika kubadilisha Sheria na Masharti haya kutokana na sababu kadhaa ikiwemo kushughulikia michezo mipya au huduma ambazo huenda tukaongeza siku zijazo, kutokana na sababu za kibiashara, ili kuambatana na sheria au kanuni, kufuata maagizo, maelekezo au mapendekezo kutoka kwa asasi inayodhibiti au kwa ajili ya kuwahudumia wateja. Sheria na Masharti mapya yanaweza kupatikana kupitia kwa kiungo cha Sheria na Masharti kwenye sehemu ya chini kabisa ya Tovuti.

Huenda tukabadilisha, rekebisha au ondoa ;huduma mojawapo au sehemu ya kuweka bet au kucheza kutoka kwa Huduma zetu kwa hiari yetu wakati wowote na tunaweza kubadili bei,  sifa maalum, uwezo, utendakazi na/au tabia za bet, michezo na/au Huduma.

KODI
Kuna kodi ya 10% kwenye ubashiri wa michezo na bonasi ya malimbikizo na 15% kwa Jackpots.